Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:11

Waziri mkuu wa Ethiopia azuru Olkaria, Naivasha


Waziri mkuu wa Ethipoia Hailemariam Desalegn.
Waziri mkuu wa Ethipoia Hailemariam Desalegn.

Kenya inanuia kushirikiana na Ethiopia kwenye sekta ya utoaji wa umeme kutokana na mvuke kwa nia ya kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili. Hayo yalisemwa mapema Ijumaa baada ya waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn kutembelea kituo cha kutoa umeme huo cha Olkaria karibu na mji wa Naivasha.

Wakati wa ziara hiyo, waziri wa kawi nchini Kenya Charles Keter alisema kuwa miradi inayohusiana na nishati baina ya Kenya na Ethiopia ndio ajenda kuu waliojadilia. Alisema kuna mipango ya kusafirisha umeme kutoka Naivasha hadi Ethiopia kwa umbali wa kilomita 600 upande wa Kenya, na kilomita 400 upande wa Ethiopia.

XS
SM
MD
LG