Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 14:51

Millioni ya watu kuathiriwa na El Nino Afrika Mashariki


El Nino Afrika
please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu milioni 18 katika ukanda wote wa Afrika Mashariki wapo katika hatari ya kukumbwa na upungufu wa chakula kutokana na hali ya hewa inayosababisha El Nino.

Muungano wa Afrika Mashariki IGAD umeonya jana Jumatano kwamba kuendelea kwa ukame unaoathiri Afrika mashariki na kati utaendelea kwa angalau miezi mitatu ijayo.

Mkurugenzi wa kituo cha utabiri wa hali ya hewa na kushughulikia masuala ya hali ya hewa cha IGAD, Guleid Artan anasema mataifa ya Afrika mashariki yatapata mvua nyingi lakini mpaka hapo mwezi Machi.

Artan anasema, ukame katika upande wa kaskazini utaendelea mpaka msimu ujao wa mvua wakati mvua zitapungua katika nusu ya kenya lakini itaptaa mvua za wastani Kusini na Magharibi mwa Kenya na Uganda, Tanzania hasa katika ukanda wa maziwa makuu.

El Nino ni suala la hali ya hewa linatokea pale viwango vya joto katika ukanda wa kati na mashariki mwa bahari ya Pacific vinakuwa na hali ya joto kali kuliko wastani na kusababisha kubadilika kwa mzunguko wa hali ya hewa ya dunia.

Madhara ya El Nino yalihisiwa mpaka mashariki mwa Afrika katika kipindi cha mwanzoni mwa mwezi Mei wakati hali ya ukame ilipoathiri sehemu za Ethiopia, Sudan na Somalia.

Kwa mujibu wa Pete Manfield kutoka ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu masuala ya kibinadamu OCHA inakadiria watu milioni 18.5 wapo hatarini kukabiliana na njaa kutokana na ukame na migogoro katika ukanda huo.

Manfield anasema, kuna idadi kadhaa ya migogoro mbalimbali katika ukanda huo ambayo ni mipya kwa mwaka huu ambayo inaongeza mahitaji mapya ya misaada ya kibinadamu kasa migogoro ya Burundi, Sudan Kusini na Yemen ambayo yote inahitaji juhudi kubwa za kipindi kifupi kukabiliana nayo ili kuokoa maisha.

Ukame katika ukanda huo umeikumba Ethiopia kwa kiwango kikubwa na serikali inaomba msaada wa dola bilioni 1.1 kusaidia kuwalisha zaidi ya watu milioni 10.

Nchi za jirani za Sudan Kusini na Somalia zote kwa pamoja zina mapambano ya ndani pamoja na ukame.

Msemaji wa mpango wa wa chakula duniani WFP Challis McDonough anasema mapambano yanaweka ugumu kwa mashirika ya misaada kuwafikia wale wenye shida.

Bi McDonough anasema, mpaka sasa ukijumuisha na hali ya mvua isiyo na uhakika na mavuno ya baadhi ya sehemu ambazo hazina migogoro ambayo imekuwa ni wagavi wa chakula kwa Sudan Kusini hali si nzuri kama tulivyotarajia…tunadhani nchini Somalia wanakumbana na

hali kama hii ambayo ni mchanganyiko wa masuala yanayohusu na migogoro.

Imekadiriwa kuwa watu 300,000 katika ukanda wa Afrika Mashariki wamekimbia makazi yao kutokana na ukame.

XS
SM
MD
LG