Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 19:47

Tishio la Ebola Kenya


Picha ya mfano wa virusi vya Ebola
Picha ya mfano wa virusi vya Ebola

Ugonjwa wa Ebola umeuwa mtu mmoja mjini Nairobi na watu kadhaa wengine wamewekewa karantini

Mwanamke mmoja amefariki nchini Kenya, Alhamis kutokana na kile kinachodhaniwa kuwa homa hatari ya ugonjwa wa Ebola.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 alitambulishwa kwa jina la Gladys Muthoni, alifariki ndani ya teksi wakati anakimbizwa kwenda hospitali ya Kenyatta mjini Nairobi.

Daktari J. Masika Wafula, anasema mgonjwa huyo alikuwa akitokwa damu mdomoni, puani na masikioni, hali inayoashiria maambukizo ya kirusi cha homa ya Ebola.

Iliwachukua saa kadhaa timu ya waauguzi kumwondoa mwanamke huyo kutoka ndani ya teksi kwa hofu ya kuambukiza watu wengine ugonjwa huo, ambao ni rahisi mno kuambukiza. Watu watatu waliokuwa wamefuatana na mgonjwa huyo, pamoja na dereva wa teksi, wote wamewekewa karantini ndani ya hoteli moja mjin humo.

Daktari Wafula hakuweza kuthibitisha kama mwanamke huyo alipata homa ya Ebola lakini anasema hospitali inalichukulia tukio hilo kama hali ya tahadhari kwa afya ya umma.

“Anasema ndio sababu walichakua tahadhari, na kuwawekwa watu waliofuatana nae katika karantini, na kuendelea na uchunguzi wa kifo hicho”.

Dada wa marehemu, Rachel Wairimu, alikwenda hospitalini hapo haraka Alhamisi baada ya baba yake kumpigia simu na kumweleza kuwa dada yake amefariki. “Anasema mara ya mwisho alizungumza na dada yake siku ya Jumapili ambapo walijadili iwapo wasafiri pamoja kwenda nyumbani kwa ajili ya krismas”.

XS
SM
MD
LG