Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 23:51

Hali ya usalama yashuhudiwa katika mtaa wa Eastleigh, Nairobi.


Wakazi wa Eastleigh wakiendelea na shughuli za kibiashara.
Wakazi wa Eastleigh wakiendelea na shughuli za kibiashara.
Baada ya siku nyingi za umuagikaji wa damu na mashambulizi ya kigaidi katika mji mkuu wa Nairobi na hususan mtaa wa Eastleigh,mashariki mwa Nairobi,hali imeanza tena kuwa shwari na maisha yanarudia hali yake ya zamani.Siku kadhaa zilizopita,maonyesho ya kimataifa ya kibiashara yalifanyika katika mtaa huo wa Eastleigh na kuhudhuriwa na wafanya biashara kutoka eneo lote la Afrika Mashariki.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:24 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Tangu majeshi ya Kenya kuingia nchini Somalia kukabiliana na magaidi a Al Shabaab karibu miaka minne iliyopita,sehemu nyingi nchini Kenya,hususan mji mkuu wa Nairobi zimeshindwa kuishi kwa amani na visa vya mauaji,umwagikaji wa damu,uharibifu mkuba wa mali vimeshuhudiwa karibu kila mahali.
Hali hii imekumba zaidi mtaa a Eastleigh,wenye idadi ya watu wasiopungua laki nne-wengi wakiwa wa asili ya Kisomali.
Lakini licha ya biashara kubwa inayoendela kunoga na kushamiri katika mtaa huo wenye bidhaa nyingi za bei nafuu na kuhudhuriwa na wateja kutoka Uganda,Tanzania,South Sudan,DRC na maeneo ya Maziwa Makuu,mtaa huo umekuwa hatari kwa mashambulio ya kigaidi.
Watu wamekuwa wakiuawa kiholela,kujeruhiwa vibaya na kukosa amani.
Lakini sasa hali imebadilika na amani imetanda kote kama kulingana na chifu wa eneo hilo Mama Jawahir Mussa..
XS
SM
MD
LG