Kenya imetangaza Jumapili mlipuko wa homa ya manjano baada ya watu watatu kufa huku kukiwa na kesi nyingie 15 zinazoshukiwa ni za ugonjwa huo, katika kaunti ya kaskazini ya Isolo.
Wizara ya Afya imesema imepeleka jopo la wataalamu katika eneo hilo kutathmini hali hiyo.
Pia imesema itatoa kipaumbele cha chanjo katika nusu darzeni ya majimbo ya karibu ambayo sasa yamewekwa katika tahadhari ya juu.
Vyombo vya habari vya ndani ambavyo viliripoti homa ya manjano kwa mara ya kwanza mwezi Januari kwenye maeneo ya Merti na Garba Tula, hali iliyozusha maswali ya kwa nini tahadhari ilitolewa Jumamosi tu.
Taarifa zinasema, lakini haya ni maeneo magumu na yaliyoko mbali nchini humo, ambako familia zinafuga wanyama, zina hama hama kutoka sehemu moja kwenda nyingine wakitafuta malisho na maji.
Vituo vya afya pia ni duni havina wafanyakazi na vifaa vya kutosha.
Homa ya manjano inaelezewa kuwa virusi vyake vinaenea kwa mwanadamu kutoka kwa mbu.
Dalili zake ni pamoja na homa kali, kichwa kuuma, macho kubadilika kuwa ya njano na wakati mwingine inasababisha maini kushindwa kufanya kazi.