Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 17:01

Taiwan inaishutumu China kuwateka raia wake kutoka Kenya


Maafisa wa Taiwan

Taipei inaishutumu China kwa kuwateka nyara raia wake 45 kutoka Kenya hatua ambayo wachambuzi wanasema huenda inalenga kukishinikiza chama tawala cha Taiwan kuanza mazungumzo ya kirafiki na China bara kinyume na msimamo wa kujitangazia utawala jambo ambalo ni kinyume na utashi wa beijing.

Kurudishwa China kwa raia hao wa Taiwan kutoka Kenya kunaelezewa na serikali ya Taiwan kuwa ni utekaji nyara wa raia wake na kudai hilo limeratibiwa na China na Kenya imetekeleza hatua ambayo wachambuzi wanasema mbinu dhidi ya Taiwan, kutokana na kisiwa hicho kuitisha uchaguzi wa rais Januari 16.

China inaiona Taiwan kuwa sehemu ya eneo lake tangu wakomunisti waliposhinda kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe katika miaka 1940 huku China ikiendelea kuhimiza kuwa lazima pande zote ziungane.

XS
SM
MD
LG