Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 15:17

Kenya kuwasafirisha raia zaidi wa Taiwan kwenda China


Ramani ya Taiwan
Ramani ya Taiwan

Kenya inajitayarisha kulihamisha kundi jingine la raia wa Taiwan hadi nchini China, baada ya kuchukua hatua kama hiyo wikiiliyopita, jambo ambalo limepelekea Taiwan kudai kwamba Beijing imewateka nyara raia wake.

Afisa wa wizara ya mambo ya nje ya Taiwan anayeshughulika na maswala ya Asia Magharibi na bara la Afrika, Antonio Chen, amesema watu 37 raia wa Taiwan waliwasili nchini China kwa ndege iliyowasafirisha kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Chen alisema baada ya watu kumi na tano kukataa kuondoka kwenye kituo cha polisi kuelekea kwenye uwanja wa ndege, polisi wa Kenya walitumia gesi ya kutoa machozi kwenye chumba walimokuwa wamezuiliwa .

Raia hao 37 wa Taiwan, ambao watasafirishwa siku ya Jumanne, pamoja na wengine nane waliofukuzwa nchini Kenya wiki iliyopita, walikamatwa mnamo mwaka wa 2014 na kushtakiwa kwa makosa ya uhalifu wa kimitandao.

Mahakama moja nchini Kenya haikuwakuta na hatia lakini ikaamuru kwamba waondoke nchini humo katika muda wa siku ishirini na moja.

XS
SM
MD
LG