Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:11

Sakata la ardhi lagubika uchaguzi wa Kenya


Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Hekaheka za uchaguzi wa Agosti 2017 nchini Kenya zimepamba moto huku suala la ardhi likiendelea kuwa ni kero miongoni mwa wakenya.

Juhudi za serikali ya chama cha Jubilee kutoa hati kwenye makazi yasiyopimwa kwa mamilioni ya wakenya wasiomiliki ardhi nchini, zimeibua hisia mchanganyiko nchini humo.

Mwandishi wa Idhaa ya Kiswahili VOA, Amina Chombo ameripoti kuwa suala la ardhi nchini Kenya limekuwa likitumiwa na wanasiasa kuwashawishi wapiga kura.

Wanasiasa wamekuwa wakiahidi kutatua mizozo ya ardhi ikiwemo kuwapa hati za ardhi wale wanaoishi katika maeneo yasiyopimwa.

Taswira ya serikali ya Jubilee imekabiliwa na changamoto kubwa baada ya ilani ya chama tawala kuidhinisha kutoa hati miliki za mashamba kwa wananchi, hati ambazo zimekabiliwa na matatizo mengi.

Hii ni baada ya uamuzi wa mahakama kuu nchini Kenya kusema kuwa zaidi ya hati miliki za ardhi milioni 3 zilizotolewa na serikali ya Jubilee tangu mwaka 2013 hazikufuata utaratibu.

Jaji wa mahakama kuu, Justice Onguto katika uamuzi wake alisema kuwa Wizara ya Ardhi nchini, iliendeleza utoaji wa hati miliki hizo bila kuhusisha Tume ya Taifa ya Ardhi ambayo ina mamlaka ya kutayarisha hati hizo, na kuipa serikali mwaka mmoja kurekebisha hilo.

Mwenyekiti wa tume ya taifa ya ardhi nchini, Profesa Mohammed Swazuri ameiambia sauti ya Amerika kwamba uamuzi wa mahakama umeambatanishwa na tangazo lao la awali.

Waziri wa ardhi nchini, Prof Jacob Kaimenyi amesema kwamba hati miliki hizo ni halali na hazina hitalafu yoyote na kuwa wizara itarekebisha makosa, kauli hiyo imepingwa vikali na wanasiasa wa mrengo wa upinzani.

XS
SM
MD
LG