Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 09:05

KDF yasema lazima kubuni amani ya kudumu nchini Somalia


Wanajeshi wa Kenya wakijiandaa kupanda lori kuelekea Liboi, Kenya karibu na mpaka na Somalia
Wanajeshi wa Kenya wakijiandaa kupanda lori kuelekea Liboi, Kenya karibu na mpaka na Somalia

Majeshi ya Kenya yasema maeneo yaliyodhibitiwa na al-Shabab nchini Somalia yapatiwe amani ya kudumu

Majeshi ya Kenya yanasema ni lazima kubuni hali ya kudumu ya amani katika maeneo ambayo awali yalidhibitiwa na al-Shabab, kabla ya kuendelea mbele kwenye ngome za wanamgambo hao.

Abdullahi Sheikh Ahmed, mzee huko Tabda kusini mwa Somalia bado ana uchunguzi kuwa si muda mrefu uliopita, wakati wanamgambo wa al- shabab walikata ugavi wa mafuta kwa mji huo, mkakati unaotumiwa na kundi la kiislamu kuwatoza kodi watu katika maeneo wanayoyadhibiti. “Anasema kundi la wazee waliomba mkutano na wawakilishi wa al-shabab katika eneo hilo na waliwasihi kwa siku kadhaa kuruhusu walau kupeleka hata punda mmoja aliyebebeshwa chakula.”

Majeshi ya usalama ya Kenya-KDF, yalichukua udhibiti wa Tabda katika hatua za awali za vita vya Kenya dhidi ya al-shabab. Tangu wakati huo, Ahmed anasema wameweza kuanzisha tena biashara na mji wa karibu wa Dobley, ili kupata mahitaji wanayoyataka.

Brigedia wa KDF, Johnson Ondieki, anasema kitu muhimu sana ni jinsi ya kuhakikisha usalama katika maeneo ambayo tayari yamekombolewa kabla ya kuingia katika awamu nyingine na tunaamini, punde tu, tutakuwa Kismayo.
Kismayo mji wa bandari wenye wakazi takriban 200,000 ni ngome kuu ya al-shabab na kituo cha muda cha kupitisha silaha na fedha. Kenya imesema tangu waanze operesheni nchini Somalia mwezi October, mwaka jana kufika kismayo ilikuwa muhimu ili kukata mitandao ya kifedha kwa kundi hilo.

Kenya inategemea mamlaka za wasomali katika maeneo hayo katika kuleta amani kwenye maeneo yaliyokombolewa. Huko Dobley, karibu na mpaka wa kenya, wanajeshi wa kisomali wanafanya kazi pamoja na wanajeshi wa Ras Kamboni, wanaoongozwa na Ahmed Madobe ambaye anasema anataka kuwawezesha wasomalia wa huko. “Madobe anasema kama kuna mtu ana mtizamo wa kisiasa wangependa kumkaribisha na kuwapa fursa watu walioko huko kuleta amani na kufanya maamuzi yao.”

Makamanda wa KDF wanasema mapigano dhidi ya al-shabab yamebadilika tangu kuanza kwa vita. Badala ya makabiliano ya ana kwa ana, wanasema wanamgambo hivi sasa wanafanya mashambulizi wakiwa katika makundi madogo madogo, hasa nyakati za usiku, wanatumia silaha nyepesi au kutegua milipuko.

Mwanajeshi mmoja ambaye alikataa kutoa jina lake amesimama nje ya hospitali moja mjini humo akilinda. Katika kofia yake kulikuwa na maneno yaliyoandikwa tunapeleka miili mbinguni.

KDF inatarajiwa kuungana na jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia-AMISOM, ambalo lina wanajeshi kutoka Uganda, Burundi na Djibouti.

Wanajeshi wa Ethiopia pia wameingia nchini Somalia kutokea upande wa magharibi, na kuweka shinikizo kwa al-Shabab katika mikoa ya kati ya Bay na Bakool ambako wanamgambo wapo.

XS
SM
MD
LG