Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 19, 2025 Local time: 05:51

Katibu mkuu wa OPEC afariki dunia


Katibu mkuu wa OPEC Mohammad Barkindo
Katibu mkuu wa OPEC Mohammad Barkindo

Serikali ya Nigeria pamoja na shirika la kimataifa la nchi ambazo zinazlisha mafuta OPEC, wamedhibitisha kifo cha katibu mkuu wake Mohammad Barkindo kilichotokea Jumanne jioni mjini Abuja.

Wizara ya mafuta ya Nigeria imeliambia shirika la habari la AP kwamba Barkindo mwenye umri wa miaka 63 aliaga muda mfupi baada ya kukutana na rais wa Nigeria Muhhamadu Buhari .

OPEC yenye makao yake makuu mjini Vienna imedhibitisha kifo hicho bila kutoa maelezo zaidi. Kifo chake kimeshtua wadau kwenye sekta ya mafuta ulimwenguni wakati akikaribia kukamilisha muhula wake wa pili hapo Julai 31, wadhifa ambao ameushikilia kwa miaka 6 tangu mwaka wa 2016.

Habari za kifo chake zilitolewa kwa mara ya kwanza kupitia ujumbe wa twitter na mkurugenzi wa shirika la kitaifa la mafuta la Nigeria, Mele Kyari. Taarifa ya OPEC imesema kwamba maneno yake ya mwisho kwa rafiki zake yalikuwa kwamba amefurahi kukamilisha muda wake kama katibu mkuu, na kwamba alifanya kila awezalo kulitumikia shirika hilo, huku pia akiwasifu waliofanya kazi naye.

XS
SM
MD
LG