Katibu mkuu wa NATO Jens Stoltenberg ameiambia pia AP katika mahojiano kwamba muungano huo, ingawa haushiriki katika vita, utaiunga mkono Ukraine“kwa muda mrefu utakaohitajika.”
Akiulizwa iwapo NATO ina dalili zozote kwamba China inaweza kuwa tayari kutoa silaha au msaada mwengine kwa vita vya Russia, Stoltenberg amesema “ Tumeona baadhi ya ishara kwamba wanaweza kupanga hilo na bila shaka washirika wa NATO, Marekani, wamekuwa wakionya dhidi ya hilo kwa sababu ni jambo ambalo halipaswi kutokea. China haipaswi kuunga mkono vita haramu vya Russia.”