Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 15:05

Katibu mkuu UM afurahishwa na makubaliano ya mgogoro wa Ethiopia


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha makubaliano ya jana baina ya makamanda wa juu wa jeshi la Ethiopia na kundi la TPLF na kuweka mazingira ya kuweka mwafaka na kutekeleza mpango wa kudumu wa kusimamisha mapigano.

Taarifa ya Jumapili inasema Katibu Mkuu Antonio Gutteres, amesisitizia utayari wa Umoja wa Mataifa kusaidia mchakato huo muhimu.

Ametoa mwito wa kuendelea mbele na jambo hilo muhimu katika kuyafanyia kazi makubaliano na kuyatekeleza ili kuboresha maiasha ta raia ikijumuisha kuongeza kasi kwa usambazaji wa misaada ya kibinadamu na kurejeshwa kwa huduma muhimu za kijamii.

Wakati huohuo, kufuatia kutiwa saini kwa makubaliano ya amani baina ya serikali ya Ethiopia na waasi wa mkoa wa Tigray, kile kilichobaki ni muhimu zaidi katika misaada ya kibinadamu na yale yanayohitajiwa kwa sana, amesema msemaji wa waasi Jumapili.

Makubaliano yalifikiwa mjini Pretoria Afrika Kusini, Novemba 2 na kutolewa mwito wa kuweka silaha chini kwa waasi na kuwezesha kufikishwa kwa misaada ya kibinadamu.

Kurejea kwa misaada Tigray, kwa watu wake milioni sita ilikuwa ni moja ya masuala muhimu ya maafikiano.

Eneo la kaskazini la Ethiopia lilikuwa katika mahitaji makubwa ya haraka ya msaada wa kibinadamu kutokana na kukosekana kwa chakula na dawa, na huduma muhimu za kijamii ikijumuisha umeme, benki na mawasiliano.

Makubaliano hayo yalifuatiwa na mazungumzo katika mji mkuu wa Kenya ili kutekeleza makubaliano ya Amani na kumaliza vita vya miaka miwili kaskazini mwa Ethiopia.

XS
SM
MD
LG