Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 23, 2025 Local time: 17:57

Karibu raia 8,500 wameuawa nchini Ukraine tangu uvamizi wa Russia kuanza-UN


Umoja wa Mataifa Jumanne ulisema idadi ya vifo vya raia vilivyothibitishwa nchini Ukraine tangu Russia ianzishe uvamizi wake inakaribia 8,500, huku kukiwa na uwezekano kuwa idadi ya kweli ni kubwa zaidi.

Ofisi ya Kamishna mkuu wa Umoja wa mataifa wa haki za binadamu ilisema katika taarifa kwamba pamoja na waliouawa, imethibitisha zaidi ya raia 14,000 walijeruhiwa.

“OHCHR inaamini kwamba takwimu halisi ni kubwa zaidi kwani upokeaji wa taarifa kutoka maeneo ambapo mapigano makali yamekuwa yakiendelea umecheleweshwa, na ripoti nyingi bado zinasubiri kuthibitishwa,” shirika hilo limesema.

Umoja wa mataifa umesema katika siku tisa za kwanza za mwezi Aprili ulithibitisha vifo vya raia 44.

Ukraine ilikabiliwa na mashambulizi ya Russia kwa miezi kadhaa wakati wa msimu wa baridi yakilenga miundombinu yake ya nishati, kwa kile Kyiv ilisema ni jaribio la Moscow kuwakatisha tamaa Waukraine kwa kukata umeme na maji katika nyumba na biashara zao.

XS
SM
MD
LG