Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 17:09

Karibu 2021


Ulimwengu umekaribisha mwaka 2021 kwa shauku kubwa, lakini sherehe za kuukaribisha mwaka mpya zilikosa mbwembwe kutokana na kuwepo hatari ya kuambukizwa virusi vya Corona.

Miji kadhaa ilifuta sherehe za kuadhimisha mwaka mpya huku viongozi wakiwahimiza watu kusherehekea mwaka mpya kwa njia salama.

Mji wa New York, hapa Marekani, ambao kwa kawaida huwa na shughuli nyingi za kusherehekea mwaka mpya, ulikuwa na shughuli chache sana na kukosa maandhari yake.

Maafisa wa usalama walikuwa wachache sana mjini humo, chini ya asilimia 80.

Katika baadhi ya nchi kama Ufaransa, Italy, Uturuki, Latvia, Jamhuri ya Czech na Ugiriki, maafisa waliweka masharti ya kuzuia watu kutoka nyumbani kwao usiku.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG