Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 27, 2025 Local time: 02:41

Kansela wa Ujerumani akasirishwa na maneno ya Rais wa Palestina


Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ambaye amekarishwa na maneno ya kiongozi wa Palestina.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ambaye amekarishwa na maneno ya kiongozi wa Palestina.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz, Jumatano amepinga alichosema kuwa ni maoni ya rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kupuuzia mauaji ya kimbari dhidi ya wayahudi.

Rais Abbas, aliulizwa wakati wa ziara yake mjini Berlin, Jumanne kuhusu maadhimisho yajayo ya miaka 50 ya shambulizi lililofanywa na Wa-Palestina dhidi ya Wa-Israel katika Olympic ya Munich.

Rais Abbas, alizungumza kuhusu matukio ambayo Wa-Israel waliwauwa Wa-Palestina toka mwaka 1947, kwa kusema Israel imeshafanya mauaji ya wengi mara 50 katika vijiji vya Palestina na miji, ndani ya Deir Yassin, Tantura, Kafr Qasim, na maeneo mengine.

Kansela Scholz ambaye alikuwepo na Abbas, wakati anatoa maoni hayo katika mkutano na wanahabari wa pamoja, alitumia ujumbe wa Twitter Jumatano ukisema alikasirishwa sana na kauli ya kiongozi wa Palestina.

XS
SM
MD
LG