Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:16

Kansas City Chiefs yatwaa Super Bowl LVII


Timu ya Kansas City Chiefs imeifunga Philadelphia Eagles na kutwaa ubingwa wa ligi ya American Football katika mchezo maarufu wa Super Bowl LVII, mjini Glendale, Arizona.

Mpaka firimbi ya mwisho matokeo yalikuwa Chiefs 38, Eagles 35.

Mchezaji kinara wa Chiefs, Patrick Mahomes, ambaye alielekea Arizona kwenye mchezo huu akiwa na jeraha la kifundo cha mguu, alifanikiwa kuziepuka mbinu timu ya Philadelphia Eagles ambayo ilitawala mchezo kwa kiwango kikubwa katika kipindi cha kwanza.

Mchezo wa Super Bowl LVII ambao ndio maarufu zaidi Marekani, ulimjumuisha mwanamuziki Rihanna, aliyetumbuiza wakati wa mapumziko na kuzua mjadala na tetesi kwamba pengine ni mjamzito wa mtoto wake wa pili.

Kama ilivyo utamaduni wa NFL, Super Bowl LVII iligubikwa na matangazo ya biashara ya kuvutia na yenye ubunifu mkubwa wakati wa matangazo ya televisheni ya moja kwa moja.

Ushindi wa Chiefs umekuwa wa pili katika misimu minne mfululizo iliyopita, na kuifanya timu hiyo kutoka jiji la Kansas City kuwa moja ya timu vigogo kwa sasa katika ligi ya NFL, chini ya kinara Patrick Mahomes.

Hongera Kansas City Chiefs,

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG