Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 17:51

Kanisa la St.Mary la Sudan Kusini latoa msaada wa kibinadamu


Watu waliokoseshwa makazi huko Sudan Kusini.
Watu waliokoseshwa makazi huko Sudan Kusini.

Kanisa moja lijulikanalo St.Mary Help of Christians Cathedral nchini Sudan Kusini hivi sasa linawasaidia zaidi ya wasudan kusini 8,500 ambao wamekimbia mapigano kwenye mji wa Wau tangu ghasia zilipozuka huko mwezi Juni.

Kanisa hilo ni kama taasisi inayofuata imani ya kidini pia linaweza kutoa msaada wa kibinadamu wakati wa matatizo linahitajika kusimama na watu wae, alisema Francis Mogga, ofisa wa kambi. Lakini St.Mary au Cathedral IDP Center imekuwa zaidi ya nyumba ya kiimani kwa watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi ambao wamezileta familia zao kuishi kwenye eneo la kanisa hadi watakaporejea nyumbani kwao. Jirani na mji huo ni eneo la umoja wa mataifa la kulinda raia -POC ambalo linahudumia watu 29,000.

Na wengi wao wanashukuru msaada wanaoupata, huku wakisema wangependa kuwa nyumbani. Maafisa wa kambi wanasema wanawahudumia zaidi ya IDPs 3,600 kwenye maeneo mengine matatu ya kanisa kuzunguka wau. Licha ya changamoto zilizopo, maafisa wanasema wataendelea kufanya hivyo hadi hali itakapokuwa salama kwa watu kuondoka.

XS
SM
MD
LG