Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:49

Kampuni ya India yasalimu amri ya Trump


Kampuni ya Infosys
Kampuni ya Infosys

Kampuni ya teknolojia yenye makao yake huko India, Infosys, imesema Jumanne kuwa itatoa fursa ya ajira 10,000 nchini Marekani, ikikuza athari ya soko lake la Marekani wakati ambapo imekuwa ikilengwa kisiasa nchini Marekani.

Infosys ndiye mtumaiji mkubwa wa visa aina ya H1-B Marekani, programu inayotumiwa na makampuni ya nje, hasa kampuni zinazohusika na teknolojia, ambazo huwaleta wafanyakazi wa kigeni Marekani baada ya biashara za nje nchini kutangaza kuwa hawawezi kuwapata wafanyakazi wenye sifa ndani ya Marekani.

Wale wanaoikosoa programu ya visa hiyo wanasema makampuni ya kigeni yamewanyang’anya wazawa kazi zao katika soko lao, lakini kwa sababu makampuni ya kigeni kwa kawaida wanalipa wafanyakazi wa muda kiwango cha chini kuliko kile ambacho wangewalipa wafanyakazi wa Marekani kufanya kazi kama hiyo.

Ikiwa ni sehemu ya kwanza ya ahadi yake kuwa “Amerika Kwanza” Rais Donald Trump hivi karibuni ameagiza mawakala wa serikali kuiangalia upya programu hiyo ya visa.

Trump amesema anataka kuleta wafanyakazi “bora na mahiri zaidi” wa kigeni na kuzifanyia marekebisho sheria za uhamiaji zinazohusiana na kazi na usalama wa mpakani. Lakini moja ya marekebisho—ni makampuni yanayolipa mishahara ya juu wapatiwe visa za kazi—ambayo itawaathiri moja kwa moja Infosys.

Idara ya Huduma ya Raia na Uhamiaji Marekani, ambayo inasimamia utoaji visa, imesema kuwa takriban asilimia 70 ya visa aina ya H1-B 85,000 zinazotolewa kila mwaka zinachukuliwa na raia wa India, na zaidi ya nusu ya hao wanafanya kazi kwenye makampuni ya Teknohama (IT) kama vile Infosys, ambayo wanawatafutia kazi wafanyakazi hao kwenye makampuni ya Marekani.

Infosys ni mmoja wa watumiaji wakubwa wa program ya visa ya H1-B, ikiwapeleka wafanyakazi zaidi ya 15,000 Marekani katika miaka miwili iliyopita, japokuwa imepunguza maombi yake ya visa kwa mwaka huu. Chini ya programu hiyo, wafanyakazi wakigeni kawaida wanaweza kuajiriwa kwa miaka mitatu na kampuni inayowadhamini na pengine hata kuomba kuongezewa muda huo.

Infosys imesema itaajiri wafanyakazi wa Marekani 10,000 kwa kipindi cha miaka miwili ijayo, ikifungua vituo vya teknolojia vinne na cha kwanza kitakuwa katika jimbo la Indiana, ambako Makamu wa Rais Mike Pence alikuwa gavana kabla ya Trump kumteua kuwa mgombea mwenza katika kampeni za siasa za kitaifa mwaka jana.

Mkurugenzi Mkuu wa Infosys Vishal Sikka ameiambia Reuters, “Ukweli ni kuwa kuwaleta raia wa Marekani wenye vipaji na kuwachanganya na vipaji vya kimataifa katika zama hizi tulizonazo na katika kipindi tunachokwenda nacho, ni jambo la busara kulifanya. Liko nje ya utegemezi wa kanuni na visa.”

XS
SM
MD
LG