Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 15:26

Kampuni ya Twitter yawaachisha kazi wafanyakazi wake 200


Nembo ya Twitter na picha ya mmiliki wake Elon Musk
Nembo ya Twitter na picha ya mmiliki wake Elon Musk

Kampuni ya Twitter imewaachisha kazi takriban wafanyakazi 200, karibu asilimia 10 ya wafanyakazi wake wote, gazeti la New York Times liliripoti Jumapili, ikiwa hatua ya hivi karibuni ya kupunguza ajira tangu Elon Musk aimiliki kampuni hiyo kubwa ya mtandaoni mwezi Oktoba mwaka jana.

Hatua hiyo ya kuwachisha kazi wafanyakazi hao 200 Jumamosi usiku iliawaathiri mameneja wa bidhaa, wanasayansi wa takwimu na wahandisi ambao walikuwa wanafanya kazi kwenye mafunzo ya mashine na usahihi wa tovuti, ambayo huwasaidia kuweka taarifa mbalimbali za Twitter mtandaoni, ripoti ya gazeti la New York Times ilisema.

Twitter haikujibu mara moja ombi la Reuters la kutoa maelezo kuhusu hatua hiyo.

Kampuni hiyo ina wafanyakazi wapatao 2.300, kama alivyosema Musk mwezi uliopita.

Hatua ya kupunguza ajira ya karibuni inafuatia kuachishwa kazi wafanyakazi wengi mapema mwezi Novemba, wakati Twitter iliwaachisha kazi wafanyakazi 3,700 katika hatua za kupunguza gharama ya matumizi ya fedha zilizochukuliwa na Musk, ambaye aliinunua kampuni hiyo kwa dola bilioni 44.

XS
SM
MD
LG