Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 11, 2024 Local time: 17:19

Kampuni ya Carrefour Kenya itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa kulipa faini ya shilingi bilioni 1.1


jiji la Nairobi, Kenya
jiji la Nairobi, Kenya

Kampuni ya biashara ya Carrefour nchini Kenya yenye makao yake Umoja wa Falme za Kiarabu, Majid al Futtaim (MAF) ilisema Jumatano kwamba itakata rufaa dhidi ya uamuzi wa kulipa faini ya shilingi bilioni 1.1 uliotolewa na mamlaka ya ushindani kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka ya ununuzi.

Mamlaka ya Ushindani ya Mdhibiti wa Kenya siku ya Jumanne ilitangaza faini hiyo, ambayo ni rekodi ya juu katika taifa hilo la Afrika Mashariki, ikisema MAF Kenya ilikuwa na hatia ya kuwapa wasambazaji bidhaa wawili wa ndani masharti yasiyofaa.

Majid Al Futtaim ina imani kamili katika usawa na uadilifu wa mazingira yetu ya biashara na inakata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mamlaka ya Ushindani kampuni hiyo ilisema katika taarifa.

Katika kufikia uamuzi wake mamlaka ilipuuza ukweli kwamba wasambazaji hao wawili wa ndani walikuwa tayari wameondoa malalamiko yao na kutia saini mikataba mipya na mfanyabaishara huyo MAF ilisema katika taarifa yake.

Forum

XS
SM
MD
LG