Mchakato wa kupeleka ndege hizo kwa wateja hatuanzishwa tena hadi FAA itakapojiridhisha kuwa kasoro hiyo imeshughulikiwa, mamlaka hiyo imesema katika ujumbe wa barua pepe, ikiongeza kuwa inashirikiana na Boeing kubaini hatua zote zinazohitajika kuchukuliwa kwa ndege zilizopelekwa kwa wateja hivi karibuni.
Jarida la Wall Street liliripoti awali kwamba Boeing haijakabidhi kwa wateja ndege aina ya Dreamliner tangu tarehe 26 Januari kutoka kwa viwanda vya utengenezaji au kutoka kwa maghala ambapo dazeni ya ndege zimehifadhiwa zikizubiri kupelekwa kwa wateja kwa sababu ya suala hilo la ukaguzi.
Facebook Forum