Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:23

Kampuni ya dawa ya Aspen ya Afrika kusini yajipanga kutengeneza chanjo zaidi za COVID-19


Mfano wa mchakato wa utengenezaji chanjo ya COVID-19
Mfano wa mchakato wa utengenezaji chanjo ya COVID-19

Aspen inakusudia kuongeza uwezo wake wa utengenezaji wa chanjo ya COVID-19 hadi dozi bilioni 1.3 kwa mwaka ifikapo Februari mwaka 2024 kutoka kwenye pato la sasa la dozi karibu milioni 250 kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Stephen Saad

Kampuni ya kutengeneza dawa ya Aspen Pharmacare ya Afrika kusini inakusudia kuongeza uwezo wake wa utengenezaji wa chanjo ya COVID-19 hadi dozi bilioni 1.3 kwa mwaka ifikapo Februari mwaka 2024 kutoka kwenye pato la sasa la dozi karibu milioni 250 mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo aliliambia shirika la habari la Reuters leo Jumatatu.

Aspen inafanya hatua za mwisho za utengenezaji wa chanjo ya Johnson and Johnson ya COVID-19 chini ya kile kinachoitwa mkataba wa kujaza na kumaliza lakini mkurugenzi mtendaji Stephen Saad alisema katika mahojiano kwamba makampuni yalikaribia kutangaza mpango mpana zaidi wa Aspen, chini ya leseni ya kuzalisha chanjo ya J&J ya COVID-19.

XS
SM
MD
LG