Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 18:10

Kampuni pekee ya umeme nchini Kenya yakosolewa kwa mpango wake wa kupunguza wafanyakazi kwa asilimia 20


Waandamanaji wakiwa na mabango katika barabara za mji wa Nairobi, wakiomba serikali kusitisha mpango wa kujenga bwawa la umeme linalotumia mkaa wa mawe. Juni 5,2018. Picha ya VOA
Waandamanaji wakiwa na mabango katika barabara za mji wa Nairobi, wakiomba serikali kusitisha mpango wa kujenga bwawa la umeme linalotumia mkaa wa mawe. Juni 5,2018. Picha ya VOA

Chama cha wafanyakazi wa kampuni ya umeme ya Kenya kimesema leo Jumatatu kwamba mpango wa kampuni hiyo wa kutaka kupunguza wafanyakazi wake kwa asilimia 20 si mzuri, kwa sababu hauzingatii mahitaji ya mtandao wa umeme kwa kutumia kazi za mikono.

Mipango ya kampuni hiyo pekee ya kugawa umeme Kenya ya kupunguza wafanyakazi wake, iliripotiwa na vyombo vya habari vya nchi hiyo mwishoni mwa jumaa, na imethibitishwa katika waraka wa kampun hiyo ambao shirika la Reuters limeuona leo Jumatatu.

Kampuni hiyo itaomba wafanyakazi 1,962 kuacha kazi kwa hiari kwa gharama ya mara moja ya shilingi bilioni 5.3, sawa na dola milioni 46.7 katika awamu tatu kufikia mwishoni mwa mwezi Juni mwaka wa 2023, waraka huo umeeleza.

Kupunguzwa kwa wafanyakazi kutaisaidia kampuni hiyo ya umeme kupunguza kiwango cha mishara ya wafanyakazi wake cha kila mwaka ambacho ni sawa na shilingi bilioni 15.8, kiwango ambacho kimekuwa kikiongezeka kwa wastani wa asilimia 12 katika miaka mitano iliyopita kufikia mwishoni mwa mwaka wa 2020, ikilinganishwa na wastani wa mapato kwa asilimia 5.4 msimu huo huo, kulingana na waraka huo.

Chama cha wafanyakazi wa kampuni hiyo ya umeme (KETAWU) kimesema mpango huo haukufikiriwa vizuri.

“Wanajaribu kulinganisha kampuni ya Kenya na kampuni kama hiyo nchini India”, katibu mkuu wa KETAWU Ernest Nadome ameliambia shirika la habari la Reuters, akiongeza kuwa sekta ya umeme nchini India inatumia zaidi mfumo wa mashini kuendeshwa na komputa kuliko Kenya.

Kampuni ya umeme ya Kenya imekataa kutoa maelezo juu ya mipango yake ya kupunguza wafanyakazi au juu ya ukosoaji wa chama cha KETAWU.

XS
SM
MD
LG