Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 01, 2023 Local time: 05:56

Kampeni za uchaguzi zapamba moto Marekani


Wagombea urais wa Marekani Hillary Clinton na Donald Trump
Wagombea urais wa Marekani Hillary Clinton na Donald Trump

Wachambuzi wa mambo wanasema mdahalo uliofanyika Jumapili ni wa kihistoria ukiwa umejaa majibizano ambayo wengine wanaona hayakuwa na manufaa kwa wananchi.

Wagombea urais wa Marekani, Hillary Clinton wa chama cha Democratic na Donald Trump wa Republican Jumatatu walirudi kwenye kampeni za urais baada ya kukutana tena uso kwa uso kwenye mdahalo wa pili wa urais uliofanyika Jumapili kwenye chuo kikuu cha Washington katika jimbo la Missouri.

Baadhi ya warepublican tayari wamegawanyika kufuatia matamshi ya Trump yaliyoonekana kwenye video iliyorekodiwa mwaka 2005 akitoa kashfa za uzalilishaji dhidi ya wanawake, na kuchochea baadhi ya wafuasi wa Republican wakimtaka ajitoe kwenye kinyang’anyiro hicho.

Wagombea wote wanafanya kampeni zaidi za kuwahamasisha wapiga kura ambao mpaka wakati huu bado hawajafanya maamuzi kwenye uchaguzi mkuu wa Novemba nane.

Wachambuzi wa mambo wanasema mdahalo uliofanyika Jumapili ni wa kihistoria ukiwa umejaa majibizano ambayo wengine wanaona hayakuwa na manufaa kwa wananchi.

Tayari hadi jumatatu usiku kura za maoni zinaonesha kuwa mgombea wa Demokratic Hillary Clinton anaongoza kwa pointi 11 dhidi ya Mrepublican Donald Trump.

Wakati huo huo, spika wa bunge la marekani, Paul Ryan aliwaambia warepublican wenzie kwa njia ya simu Jumatatu kwamba hatofanya kampeni za aina yeyote kwa ajili ya Trump au kumtetea juu ya matamshi yake yaliyosambaa hivi karibuni yanayokashfu wanawake.

Ryan alisema badala yake atalenga juhudi zake za kuhakikisha wabunge wa Republican wanachaguliwa kwa wingi kwenye bunge lijalo. Chama cha republican, kwa sasa kinadhibiti bunge kote katika baraza la seneti na wawakilishi.

XS
SM
MD
LG