Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:23

Kampeni za uchaguzi wa urais zaanza rasmi DRC


Wafuasi wa upinzani Congo wakiandamana mbele oa ofisi ya posta kinshasa
Wafuasi wa upinzani Congo wakiandamana mbele oa ofisi ya posta kinshasa

licha kuwepo malalmiko mengi kuhusu kutokuwa tayari kufanyika uchaguzi DRC , kampeni za uchaguzi wa urais zitaanza ijumaa

Kundi la kutetea haki za binadamu- Human Rights Wtch limetoa mwito kwa wagombea wa kisiasa wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo-DRC, kujiepusha na vitendo vya ghasia wakati wa kampeni za uchaguzi zinazoanza ijumaa .

Kundi hilo la kimataifa la kutetea haki za binadamu limesema limeandika dazani za matukio ya hivi karibuni ambayo yanatumiwa na wagombea katika hotuba zao za chuki ili kuchochea ghasia dhidi ya wagombea waupinzani na wafuasi wao.

Kundi hilo limesema polisi imetumia nguvu nyingi dhidi ya waandamanaji wa upinzani hivyo kuzusha hofu kuhusu uhalali wa uchaguzi wa urais wa novemba 28 na uchaguzi wa serikali za mitaa.

Rais Joseph Kabila anakabiliwa na upinzani mkali katika uchaguzi wa urais . Mmoja wa wapinzani wake wakubwa ni Ettiene Tshisekedi mwanasiasa mwenye umri wa miaka 78 aliyegomea uchaguzi wa urais wa mwaka 2008.

Mapema mwaka huu rais Kabila alieleza matumaini yake kwamba anatarajia kushinda katika uchaguzi.

Hata hivyo ameahidi kuachia madaraka kama atashindwa.

XS
SM
MD
LG