Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 19:43

Kamishna wa wahamiaji ulaya anasema Brussels huwenda ikazuia misaada


Wahamiaji wa kiafrika wakisubiri kuokolewa katika bahari ya Mediterranean. Oct. 3, 2016.
Wahamiaji wa kiafrika wakisubiri kuokolewa katika bahari ya Mediterranean. Oct. 3, 2016.

Kamishna wa uhamiaji katika Umoja wa ulaya alisema Brussels huwenda ikazuia msaada wa maendeleo na kuweka vizuizi vya biashara na visa kwa nchi za vyanzo vya wahamiaji kwa mataifa ya Afrika na Asia kuwalazimisha kuwachukua tena watu walioshindwa kupatiwa hifadhi.

Katika mahojiano na gazeti la The Times la Uingereza lililochapishwa Jumamosi, Dimitris Avramopoulos alisema wakuu wa EU wanafikiria kuacha kufadhili miradi mikubwa ya maendeleo. “Tuliwekeza katika maeneo haya kufungua fursa na kuwaweka watu huko”.

Avramopoulos alisema nchi ambazo zilishindwa kutoa ushirikiano kwa watu waliorudishwa katika nchi walizotoka zitaweza kukabiliwa na kuzuiwa kupatiwa visa.

Ujerumani karibuni ilitishia kusitisha visa kutoka nchi zenye vyanzo vya wahamiaji ambazo hazikubali watu kurudishwa.

XS
SM
MD
LG