Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 10:55

Kambi ya "La" yakiri kushindwa


Kambi ya "La" yakiri kushindwa
Kambi ya "La" yakiri kushindwa

Kambi ya "La" katika kura maoni nchini Kenya imekiri kushindwa huku takwimu zikionyesha kuwa upande wa "Ndiyo" umepata zaidi ya asilimia 70.

Kiongozi wa kundi lililokuwa likipinga katiba mpya ambaye pia ni Waziri wa Elimu ya Juu William Ruto ameongoza timu ya wanasiasa kadhaa katika tamko la kukubali kushindwa katika rasimu ya kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba nmchini Kenya iliyofanyika Jumatano.

Bwana Ruto amewapongeza Wakenya kwa kupiga kura hiyo kwa amani. Waziri huyo amesema ‘’Wakenya wamezungumza na lazima tuheshimu uamuzi wao’’, akiongeza kuwa ‘’Wakenya wote ni washindi.’’

Hata hivyo kambi la "La" imetaka kuwepo na majadiliano ya haraka kati ya pande hizo mbili kwa lengo la kumaliza utata wa baadhi ya masuala yaliyomo katika rasimu hiyo.

Bwana Ruto alikuwa amefuatana na mawaziri wenzake Naomi Shaaban na Samuel Poghisio na wabunge kadhaa waliokuwa wamejiunga katika kambi ya kupinga katiba hiyo iliyokuwa ikijulikana kama ‘’Red camp’’.

Alisema vigezo vya kimataifa vya kupitisha katiba mpya havijafikiwa bado akionyesha Wakenya wengi walihitaji kuwekwa pamoja.

"Tunataka kuwa sehemu ya kuipeleka Kenya mbele," alisema katika kusisitiza wito wake wa majadiliano zaidi na umoja wa kitaifa. Bwana Ruto amewapongeza Wakenya kwa kuonyesha ukomavu katika kufikia maamuzi licha ya kuwepo kile alichokiita uingiliaji wa nchi za kigeni na matumizi mabaya ya mali ya umma wakati wa kampeni hiyo.

Viongozi wa makanisa nchini Kenya pia wamesisitiza kuwepo kwa majadiliano zaidi katika masuala yenye utata katika katiba mpya ambayo yaliwafanya waipinge.

Katika mkutano mwingine tofauti na waandishi wa habari katika eneo hilo ambapo waliokuwa wakiipinga katiba hiyo kukiri kushindwa viongozi wa makanisa wamesema kuwa hatua za awali kabla ya kura ya maoni zilitawaliwa na ukiukwaji wa taratibu nas kanuni ambazo zimeendelea hadi siku ya kupiga kura."

"Wasiwasi wetu unasukumwa na suala kwamba ni asilimia 30 tu ya wapiga kura waliojiandikisha wamepitisha mapendekezo hayo. Katibu mkuu wa baraza la makanisa nchini Kenya Canon Peter Karanja amesema.

XS
SM
MD
LG