Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:11

Kamati za baraza la seneti zatoa ripoti juu ya shambulizi la Januari 6 bungeni


Waunga mkono wa Donald Trump, ikiwa ni pamoja na Jacob Chansley, kulia ikiwa na kofia yenye manyoya wakipambana na Polisi wa bunge la Marekani mjini Washington Dc.
Waunga mkono wa Donald Trump, ikiwa ni pamoja na Jacob Chansley, kulia ikiwa na kofia yenye manyoya wakipambana na Polisi wa bunge la Marekani mjini Washington Dc.

Kamati mbili za baraza la seneti Marekani zilitoa ripoti ya pamoja siku ya Jumanne inayoelezea makosa kadhaa ya kijasusi na kiusalama kabla na wakati wa shambulizi la Januari 6, kwenye jengo la bunge.

Januari 6,2021 haikuashiria tu shambulizi kwenye Jengo la bunge bali pia liliashiria shambulizi kwa demokrasia, inasema ripoti hiyo. Vyombo vinavyohusika na kulinda jengo la bunge na kila mtu katika eneo hilo siku hiyo hakuandaliwa kwa shambulizi kubwa licha ya kufahamu uwezekano wa ghasia kulenga jengo hilo.

Kamati za usalama na sheria za Seneti zilizindua uchunguzi wao wa pande mbili mwezi Februari, wakisikiliza ushahidi kutoka kwa wakuu wa Polisi wa Marekani katika jengo la bunge na vyombo vingine vya sheria, pamoja na maafisa wa sasa na wa zamani kutoka Idara ya Ulinzi na Idara ya Usalama wa Nchi. Kamati hizo pia zilisema zilipitia maelfu ya nyaraka na kupokea taarifa zilizoandikwa kutoka kwa maafisa 50 wa Polisi wa bunge.

XS
SM
MD
LG