Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 19:59

Kamati ya shirika la Msalaba Mwekundu yamtembelea Gbagbo


Rais wa zamani wa Ivory Coast akiwa kizuizini

Msemaji wa shirika la Msalaba Mwekundu alisema ijumaa maafisa kutoka shirika hilo walikutana na bwana Gbagbo na wengine walio kizuizini au kifungo cha nyumbani

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu imemtembelea rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo ambaye yuko kizuizini katika taifa hilo la Magharibi tangu April.

Msemaji wa shirika la Msalaba Mwekundu alisema Ijumaa maafisa kutoka shirika hilo walikutana na bwana Gbagbo na wengine walio kizuizini au kifungo cha nyumbani ili kuhakikishia kuwa wanatendewa haki baada ya ghasia za baada ya uchaguzi nchini Ivory Coast.

Ziara ya matembezi ya wiki hii ilikuwa ni pamoja na Bouna, Boundiali, Katiola, Korhogo, na Odienne.

Shirika la Msalaba Mwekundu limesema limetembelea wafungwa 500 katika vituo 60 kote Ivory Coast .

XS
SM
MD
LG