Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 12, 2024 Local time: 04:02

Kamala na Trump waunga mkono uondoaji malipo ya bahshish kwa wafanyakazi


Mgombea uRais wa chama cha Demokratik na makamu wa uraisKamala Harris (kulia) na rais wa Marekani Donald Trump. Picha na AFP
Mgombea uRais wa chama cha Demokratik na makamu wa uraisKamala Harris (kulia) na rais wa Marekani Donald Trump. Picha na AFP

Rais wa zamani Donald Trump na Makamu wa Rais Kamala Harris wana angalau jambo moja wanalokubaliana, wote wawili wanataka kuondoa kodi kwa baadhi ya malipo ya bahshish kwa wafanyakazi.

Wagombea wote wawili walitangaza msimamo wao huko Nevada, hatua ambayo ina moja ya viwango vya juu vya wafanyakazi wa huduma nchini.

Wabunge kutoka pande zote mbili pia wanaunga mkono sheria ambayo itafanya mabadiliko hayo.

Wengine wanasema mabadiliko hayo yatawasaidia wafanyakazi wanaopewa bahshish, ambao ni vijana na wale wa kima cha chini cha mshahara.

Lakini wengine wanasema mipango hiyo ina dosari na ingewashawishi wafanyakazi matajiri kama wanasheria kuhamisha fidia zao kuwa ni bahshish.

Prof. James R. Hines kutoka Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Michigan anasema kwamba bahshish mara nyingi huhesabiwa kama mapato, na kutekeleza mabadiliko itabidi Bunge liingilie kati.

Hines pia anadokeza kuwa kushughulikia masuala haya katika kampeni ya urais kunapendekeza changamoto zake.

Vyovyote vile, kuondoa ushuru kwa malipo hayo ya bahshish kunaweza kuwa rahisi kusema kuliko kutekeleza.

Forum

XS
SM
MD
LG