Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 07, 2022 Local time: 10:30

Kagame azindua wiki ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari


Rais wa Rwanda Paul Kagame (kushoto) na mkewe Jeannette Kagame (Kulia) wakitoa heshima zao kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 27 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi, Kigali, Rwanda, Aprili 7, 2021. (Photo by

Rwanda imeanza wiki ya kumbukumbu ya maombolezo ya mauaji ya kimbari yaliyotokea katika nchi hiyo miaka 27 iliyopita.

Huu ni mwaka wa pili sasa kumbukumbu za mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi wa Rwanda zikifanyika katika hali isiyo ya kawaida kutokana na kuwepo kwa janga la corona.

Zoezi limeanza mapema leo ambapo Rais wa Rwanda Paul Kagame amewaasha mshumaa wa matumaini ambapo utawaka kwa siku 100 sawa na muda ambao yalidumu mauaji hayo.

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema hakuna wakati hata mmoja ambao nchi yake imeweza kuwa pamoja zaidi ya wakati huu, lakini akasema mafanikio hayo bado yanakumbwa na changamoto kutoka kwa baadhi ya nchi za nje.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (L) na mkewe Jeannette Kagame (R) wanawasha moto wa kumbukumbu ya miaka 27 ya Mauaji wa Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 dhidi ya Kabila la Watutsi katika kituo cha kumbukumbu cha Kigali Genocide Memorial, Kigali, Rwanda, Aprili 7, 2021. (Photo by Simon Wohlfahrt / AFP)
Rais wa Rwanda Paul Kagame (L) na mkewe Jeannette Kagame (R) wanawasha moto wa kumbukumbu ya miaka 27 ya Mauaji wa Kimbari yaliyotokea mwaka 1994 dhidi ya Kabila la Watutsi katika kituo cha kumbukumbu cha Kigali Genocide Memorial, Kigali, Rwanda, Aprili 7, 2021. (Photo by Simon Wohlfahrt / AFP)

"Baadhi ya hawa watu pale walipo wakijaribu kuandaa masomo kwetu sisi, kuhusu jinsi demokrasia inavyoendeshwa na haki za binadamu. Lakini wakati huo huo unakuja wao hao hao wakiwakumbatia wale waliofanya mauaji haya tunayo yakumbuka hii leo. Wanawalinda,wanawasemea na kuwasaidia huku wakisema hawa ndiyo watu wanaotaka kuibadili Rwanda," ameeleza Kagame.

Kumbukumbu za mauajo haya zimefanyika huku kukiwepo na itikadi za mauaji hayo zinazoendelea kusikika huku na kule ulimwenguni kutoka kwa wale wanaotajwa kama wapinzani wa serikali ya Rwanda lakini ambao serikali inashikilia walihusika kwenye mauaji hayo. Rais akiwazungumzia hao pia na kwa kutumia lugha ya mafumbo amesema

Rais Kagame ameongeza kuwa : "Yaani ni jambo la kuvutia unapowaona mataifa hayohayo yakiwakamata watu hao kwa makosa kwa mfano ya ubakaji au wizi wa pesa waliofanya katika nchi hizo zilizowakumbatia na wanapofikishwa mahakamani bado utazisikia sauti zinazosema, imesababishwa na maagenti wa Kagame, hivi ni kwa jinsi gani unaweza kwenda kwenye nchi ya kigeni na kumlazimisha mtu kulifanya kosa la ubakaji au kosa la wizi? Lakini unakuta haya yote tunakuwa tumeyasema mapema bila kusikilizwa kwa sababu za kimaslahi."

Rais Paul Kagame amesema ukweli kwamba bado kuna miili ya waathirika wa mauaji inayoendelea kuokotwa hapa na pale miaka 27 iliyopita ni ishara nyingine, huku akisema serikali yake na wananchi kwa ujumla hawatakubali kufumba macho wakati waliofanya hayo wakiendelea kubeza kutokea kwa mauaji hayo.

Awali ilizoeleka watu kukusanyika katika maeneo mbalimbali lakini safari hii hilo halikuwepo kutokana na kupambana na maambukizi ya virus vya corona. Rais Kagame amesema kwamba hali hii imesababisha machungu zaidi kwa manusura lakini akawapa matumaini kwamba huenda ikaisha.

Rwanda inaendelea kutoa chanjo ya corona kwa wananchi wote hali ambayo kwa kiasi fulani imeleta matumaini miongoni mwa wananchi.Kumbukumbu zilizoanza leo zitaendelea kutimia siku mia moja muda ambao mauaji hayo yaliyoua zaidi ya watu milioni moja yalidumu.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG