Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 05:01

Kabuga mwenye umri wa miaka 87 afunguliwa mashtaka ya mauaji ya kimbari


Félicien Kabuga, anayeshukiwa kwa kuchochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda. Anatuhumiwa pia kwa kutoa mafunzo kwa kundi lenye silaha. Picha: AFP
Félicien Kabuga, anayeshukiwa kwa kuchochea mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda. Anatuhumiwa pia kwa kutoa mafunzo kwa kundi lenye silaha. Picha: AFP

Mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994, Felicien Kabuga, mwenye umri wa miaka 87, amefunguliwa mashtaka katika mahakama ya umoja wa mataifa mjini Hague Uholanzai.

Felicien Kabuga, anashutumiwa kwa kuchochea mauaji hayo na kuvuruga mipango ya serikali kusitisha mapigano.

Amekataa kuhudhuria kikao cha ufunguzi wa kesi yake hii leo, ambayo inasikilizwa miongo mitatu baada ya kutokea mauaji hayo yaliyodumu mda wa siku 100 na kusababisha mauaji ya watu 800,000.

Kabuga hakufika mahakamani kutokana na utata unaokumba uwakilishi wa mawakili wake, lakini jaji anayesimamia kesi hiyo Iain Bonomy amesema kwamba kesi hiyo itafunguliwa hata bila ya Kabuga kuwa mahakamani.

Mauaji ya watu kutoka kabila la Watutsi yalianza April 6, 1994 baada ya ndege iliyokuwa imembeba rais Juvenal Habyarimana kutoka kabila la Wahutu kuangushwa baada ya kupigwa risasi katika mji wa Kigali na kusababisha kifo chake.

Watutsi walilaumiwa kwa kuangusha ndege hiyo na makundi yenye silaha ya wahutu yalianza kuwaua Watutsi.

Waendesha mashtaka wamesema kwamba Kabuga aliunga mkono mauaji yaliyokuwa yakiendelea na kutoa mafunzo kwa kundi lenye silaha la Interahamwe, lililokuwa likiongoza mauaji hayo.

XS
SM
MD
LG