Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 19:28

Wanajeshi na Polisi wametanda katika maeneo ya mji mkuu wa DRC.


Pope Francis alipokutana na rais Joseph Kabila huko Vatican, Sept. 26, 2016.
Pope Francis alipokutana na rais Joseph Kabila huko Vatican, Sept. 26, 2016.

Wanajeshi na Polisi wametanda katika maeneo ya mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo huku kukiwa na wasi wasi wa ghasia katika siku rasmi ya mwisho ya rais Joseph Kabila madarakani.

Kabila anadhamiria kubaki madarakani baada ya siku ya mwisho ya saa sita usiku Jumatatu baada ya mahakama kuamua anaweza kuendelea kubaki madarakani mpaka hapo uchaguzi utakapofanyika.Kura iliyokuwa ifanyike Novemba imeahirishwa moja kwa moja.

Kanisa katoliki limekuwa llikisimamia mazumgumzo ya amani kati ya chama cha Kabila na upinzani , licha ya kwamba sasa mazungumzo hayo yamesitishwa hadi jumatano.

Upinzani haujaitisha maandamano ingawa wadadisi wengi wanatarajia wapinzani wa rais Kabila kuingia mitaani kuandamana kama walivyofanya mapema mwaka huu wakati tume ya uchaguzi iliposhindwa kuitisha uchaguzi huo. Makundi ya haki za binadamu yanasema watu zaidi ya 50 walifariki katika ghasia hizo.

XS
SM
MD
LG