Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 21, 2023 Local time: 08:47

Kabila aapishwa rasmi Rais wa DRC


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila

Rais Kabila ala kiapo cha kuwaongoza wakongoman kwa muhula mwingine wa miaka mitano

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo aliyeapishwa tena Jumanne kuanza awamu ya pili ya miaka mitano ameahidi kuunganisha nchi yake licha ya kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi kudai yeye ni kiongozi halali wa nchi hiyo.

Bwana Kabila aliapishwa Jumanne mjini Kinshasa kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita ambapo waangalizi wa kimataifa wanasema ulikuwa na kasoro nyingi wakati wa upigaji kura pamoja na hesabu za kura hizo.

Maafisa wa marekani pia wamesema uchaguzi huo ulikuwa na “mapungufu mengi”.
Bwana Kabila anasisitiza kuwa hakuna shaka kuhusu kuchaguliwa tena kwake, na maafisa wa uchaguzi nchini humo wanasema ameshinda uchaguzi huo kiurahisi. Lakini mpinzani wake mkuu Tshisekedi anayakataa matokeo akisema ni ya wizi na alijitangaza mwenyewe kuwa ni Rais akisema ataapishwa Ijumaa.

Bwana Kabila anamshauri Tshisekedi kutumia mfumo halali wa kisheria nchini humo kuweza kupinga matokeo hayo.

Uchaguzi huo wa urais na wabunge ulikuwa uchaguzi wa pili huru nchini Congo tangu nchi hiyo ilipojitenga miaka kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vilimalizika mwaka 2003.

Bwana Kabila alikuwa Rais kwa mara ya kwanza baada ya kuuwawa kwa baba yake mwaka 2001, na baadae alishinda kuwepo madarakani kufuatia kura iliyodhaminiwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2006.

XS
SM
MD
LG