Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 10:30

Kabila asema DRC ipo tayari kupambana na waasi wa Rwanda


Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-Moon (C) akikutanisha mikono ya Rais wa DRC,Joseph Kabila (L) na Rais wa Rwanda Paul Kagame kwenye kikao cha 67 cha UN
Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-Moon (C) akikutanisha mikono ya Rais wa DRC,Joseph Kabila (L) na Rais wa Rwanda Paul Kagame kwenye kikao cha 67 cha UN

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Joseph Kabila anasema jeshi lake lipo tayari kuwasaidia walinda amani wa Umoja wa Mataifa kupambana na waasi wa Rwanda katika majimbo ya mashariki mwa nchi yake.

Ahadi hiyo ilitolewa jumatano wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya bwana Kabila na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon. Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema kwamba Katibu Mkuu alisisitiza kwamba viongozi wa waasi wa kihutu wa Rwanda walishindwa kutimiza ahadi ya kutua chini silaha ifikapo Januari mbili mwaka huu.

Ban Ki-moon
Ban Ki-moon

Taasisi hiyo ya dunia awali ilieleza umuhimu wa kuwasaidia wanajeshi wa Congo katika kulisambaratisha kundi la waasi linalovuruga amani huko lijulikanalo kama Democratic Forces for the Liberation of Rwanda kutoka eneo la mashariki lenye utajiri wa madini.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari jumatano kwamba jeshi la Umoja wa Mataifa lijulikanalo kama MONUSCO karibu litatia saini mkataba na serikali ya Kabila kuidhinisha operesheni.

Maafisa wanasema kundi la waasi la FDLR linajumuisha wapiganaji ambao walishiriki katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ya wa-Tutsi walio wachache nchini Rwanda pamoja na wapiganaji wa Congo.

Jeshi la walinda amani la Umoja wa Mataifa lenye watu 20,000 linajumuisha kikosi cha mapigano ambacho kinakabiliana na makundi yenye silaha. Mwaka 2013 kile kinachoitwa kikosi maalumu cha Intervention Brigade kiliungana na jeshi la Congo kulitokomeza kundi lenye silaha lililogawanyika lijulikanalo kama M23.

XS
SM
MD
LG