Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 01, 2022 Local time: 04:05

Justin Amash amejitetea dhidi ya matamshi yake makali kwa Trump


Mbunge Justin Amash wa jimbo la Michigan kwa tiketi ya Republican

Ni mrepublican wa kwanza kutoa wito akitaka Rais Trump afunguliwe mashtaka kutokana na ukiukaji wa sheria kuhusu ripoti ya mwendesha mashtaka mkuu Robert Mueller iliyochunguza iwapo kampeni ya Trump ilishirikiana na Russia kuingilia kati uchaguzi Marekani 2016

Mbunge wa jimbo la Michigan nchini Marekani aliyekuwa m-Republican wa kwanza kutoa wito kwa Rais Donald Trump afunguliwe mashtaka alijitetea siku ya Jumatatu japokuwa msimamo wake ulimsababisha kushambuliwa na warepublican wengine wanaomuunga mkono Trump.

Mbunge Justin Amash anayehudumu kwa muhula wa tano bungeni aliwaeleza wakosoaji wake kwamba walieleza matamshi kadhaa ya uongo katika kudai kwamba Trump hakuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi kwa kujaribu kusitisha uchunguzi wa muda mrefu uliofanywa na mwendesha mashtaka maalumu Robert Mueller kuhusiana na Russia kuingilia kati uchaguzi mkuu wa urais Marekani 2016.

Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Wakosoaji wa uchunguzi wa Mueller akiwemo rais mwenyewe wanadai kwamba Trump hakuweza kuzuia mkondo wa sheria kufanya kazi kwa sababu hakukuwa na uhalifu wa kuzuia sheria kufanya kazi kwa kuwa Mueller aligundua kuwa sio Trump wala kampeni yake ilishirikiana na Russia kumsaidia Trump ashinde kuingia White House.

Lakini Amash alieleza kuwa wachambuzi wa sheria wa Marekani wanakubaliana kwamba kizuizi cha sheria hakihitaji hatua ya kuelezea uhalifu wenyewe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG