Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 10, 2022 Local time: 11:01

Jusa: ACT Wazalendo kuamua karibuni kama itajiunga na serikali ya Umoja Zanzibar


Ismail Jusa, afisa muandamizi wa ACT Wazalendo

Ismail Jusa anasema ni baada ya ushauriano na kutafakari juu ya maoni ya wanachama, ndipo uwongozi wa ACT Wazalendo utamua kujiunga au la na serikali ya umoja wa kitaifa kama inavyohitajika na katiba.

Naibu mwenyekiti wa chama cha upinzani cha ACT Wazalendo visiwani Zanzibar Nassor Mazrui ameachiwa huru kwa dhamana baada ya kushikiliwa na polisi tangu siku ya pili baada ya uchaguzi mkuu hapo tarehe 28 Octoba. Mazrui ameachiwa pamoja na Ayub Bakari Hamad siku moja kabla ya kusikilizwa kesi yao leo ya kutaka kuachiliwa huru. Akizungumza na Sauti ya Amerika kutoka hospitali mjini Nairobi, Ismail Jusa afisa muandamizi wa ACT Wazalendo aliyeumizwa wakati walipokamatwa Oktoba 29, anasema ni jambo zuri kwa Zanzibar na hivi sasa wataendelea na juhudi zao kudai haki kufuatia uchaguzi ambao anasema ulikua na wizi mkubwa wa kura.

Mahojiano na Ismail Jusa afisa muandamizi wa ACT Wazalendo
please wait

No media source currently available

0:00 0:06:25 0:00


Facebook Forum

XS
SM
MD
LG