Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 30, 2023 Local time: 00:05

Juneteenth: Marekani yasherehekea Sikukuu ya kumbukumbu ya kumalizika kwa utumwa


Wamarekani wakisherehekea sikukuu ya Juneteenth.

Watu nchini Marekani katika wikiendi ndefu ya mapumziko wanasherehekea “Juneteenth,” wakiadhimisha sikukuu ya kitaifa ya kumbukumbu ya kumalizika kwa utumwa baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Huu ni mwaka wa pili kwa Juneteenth, ikiwa ni kifupi cha “June19th,” imekuwa ni sikukuu ya serikali kuu.

Jumatatu, sikukuu ya serikali kuu ya Juni 19 ni kumbukumbu ya siku hiyo mwaka 1865 wakati watu waliokuwa watumwa huko Galveston, Texas, walifahamu kuwa walikuwa huru – miaka miwili baada ya Tangazo la Kuwaachia Huru Watumwa lililotolewa wakati wa vita vya umwagaji dawa vya wenyewe kwa wenyewe.

Wakazi wakihudhuria tafrija ya kuadhimisha Juneteenth huko Nashville, Tennessee, REUTERS/Kevin Wurm.
Wakazi wakihudhuria tafrija ya kuadhimisha Juneteenth huko Nashville, Tennessee, REUTERS/Kevin Wurm.

Wakati wengi wamekuwa wakiichukulia sikukuu hii ya wikiendi ndefu kama ni sababu ya kufanya tafrija, wengine wanahimiza kutafakari kimyakimya juu ya vitendo vya ghasia na ukandamizaji ambavyo aghlabu hutokea Marekani kwa raia wake Weusi.

Bado wengine wameeleza juu ya kustaajabishwa na kusherehekea sikukuu hii ya serikali kuu inayaadhimisha kumalizika kwa utumwa katika taifa wakati Wamarekani wengi wanajaribu kuzuia sehemu ya historia hiyo kufundishwa katika shule za umma.

“Je, Juneteenth ni sikukuu pekee ya serikali kuu ambayo baadhi ya majimbo imepiga marufuku kufundishwa historia yake na umuhimu wake?” Mwandishi Michelle Duster aliuliza kupitia mtandao wa Twitter wikiendi hii, akizungumzia hatua zilizochukuliwa huko Florida, Oklahoma na Alabama kupiga marufuku mafunzo ya dhana fulani juu masomo ya Wamarekani Weusi au ufundishaji wa baadhi ya nadharia za ubaguzi na ukabila.

Katika wikiendi ya Juneteenth, kanisa Katoliki huko Detroit lilitenga ibada yake kuwasihi waumini wake kuangalia kwa undani zaidi kuhusu masomo hayo kutokana na sikukuu hiyo.

“Ili kuwepo haki lazima tujitahidi kufikia Amani. Na ili kuwepo Amani lazima tufanye bidii kuwepo haki,” John Thorne, mkurugenzi mtendaji wa Ushirika wa Kiuchungaji wa Wakatoliki Detroit, aliwaambia waumini waliokusanyika kwenye ibada kwenye Kanisa Katoliki la Gesu huko Detroit.

“Mapambano bado hayakwisha. Kuna kazi kubwa ya kufanywa,” alisema.

Wamarekani Weusi wengi wanakubaliana na hilo, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni wa hivi karibuni. Asilimia 70 kamili ya watu wazima Weusi Waliohojiwa katika ukusanyaji maoni wa AP-NORC walisema “mengi” yanatakiwa kufanyika ili kufanikisha haki sawa kwa Wamarekani Weusi katika suala la sera.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.

Forum

XS
SM
MD
LG