Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 03:58

Jumuiya ya SADC yakutana DRC kuzungumzia uchumi


Mwenyekiti wa Jumuiya ya SADC anayemaliza muda wake Rais wa Malawi Lazarus Chakwera.

Wakuu wa nchi kutoka Jumuiya ya SADC wanakutana Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC, kwa ajili ya mazungumzo ya ukuzaji na kuinua uchumi.

Darzeni ya wakuu wa nchi waliwasili katika mji mkuu Kinshasa Jumanne kushiriki katika Mkutano wa siku mbili ambao umefunguliwa Jumatano.

Viongozi hao wanajadiliana jinsi ya kukuza uchumi wa viwanda, kupitia mageuzui ya kilimo, kuendeleza rasilimali za madini na mifumo ya thamani katika kiwango cha eneo.

DRC pia inatarajia kuomba msaada katika jumuiya hiyo kurejesha amani na usalama katika ardhi yake.

Lengo jingine la mkutano huo ni kukabidhi uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa Rais wa DRC Felix Tshisekedi kutoka kwa kiongozi wa sasa Rais wa Malawi Lazarus Chakwera.

XS
SM
MD
LG