Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 31, 2023 Local time: 03:53

Jumuiya ya Afrika mashariki yatoa wito kusaidia janga njaa na ukame


Jumuiya ya Afrika mashariki yatoa wito kusaidia janga njaa na ukame

Mbunge wa Afrika Mashariki bwana Fortunatus Masha anasema jumuiya hiyo imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za njaa katika pembe ya afrika

Suala la ukame siyo tu limekumba pembe ya Afrika lakini pia nchi za Afrika mashariki zimeathiriwa na janga hilo kama vile kaskazini mwa Kenya, Tanzania na Ethiopia.

Somalia ikiwa ndiyo iliyoharibiwa vibaya na njaa kutokana na ukame, mikoa ya kusini mwa Shabelle na Bakool awali ilijulikana kama mzalishaji mkubwa wa chakula lakini sasa imetambuliwa kimataifa kukumbwa na ukame na njaa.

Mbunge wa Afrika Mashariki Bw. Fortunatus Masha anasema jumuiya hiyo imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za njaa katika pembe ya afrika na amezitaka nchi husika kulinda watu wake na baa hilo.

“Ni kweli kabisa katika nchi za Kenya kaskazini na sehemu za Uganda na maeneo mbalimbali ya Tanzania hali ya chakula siyo nzuri safari hii. sisi tunawasihi viongozi wan chi hizi wafanye kila namna kuhakikisha kwamba watu hawatakufa njaa kutokana na janga la ukame.“

Somalia inayozungumziwa kwa wingi katika pembe ya Afrika ikidaiwa kuathiriwa vibaya na ukame ambao haujawahi kutokea tangu miaka 60 iliyopita umelazimisha maelfu ya watu kumiminika nchini Kenya kuomba hifadhi katika kambi za Daadab.Lakini anasema mageuzi ya kilimo ni muhimu katika baadhi ya nchi.

Katika maathiriko haya ya ukame na njaa akina mama na watoto ndio waathiriwa wakubwa . kwa mfano nchini tanzania shirika la “Save the Children” tayari limetangaza kuwa kuna maeneo mengi nchini humo yaliyokumbwa na utapiamlo kutokana na njaa.

Tayari dunia imeshachukua tahadhari za kusaidia katika janga hili la njaa na ukame hasa katika pembe ya Afrika. Mashirika ya kimataifa kama vile yale ya chakula-WHO, shirika la kuhudumia watoto-UNICEF, na shirika la kuhudumia wakimbizi –UNHCR, yote yanashirikiana kwa karibu kusaidia maelfu ya watu.

XS
SM
MD
LG