Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:44

Jumatano ni sikukuu ya Eid al Fitr


Waumini wa kiislam katika sala za wakati wa mwezi wa Ramadan.
Waumini wa kiislam katika sala za wakati wa mwezi wa Ramadan.

Waislam kote duniani wamekamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan unaofuatiwa na sherehe za Eid al Fitr. Sherehe za Eid al Fitr huangukia siku ya kwanza ya Shawwal, ikimaanisha kumalizika kwa mwezi Ramadan katika mwezi wa kumi wa kalenda ya ki-islam.

Sherehe hizi pia zinamaanisha kukamilika kwa siku 29 au 30 za kufunga ramadan ambazo waumini hufunga ikimaanisha kutokula mlo wa aina yeyote hata maji pale jua linapochomoza na kufungua pale jua linapotua ndipo waumini huanza mlo kwa kuonja tende.

Huko nchini Kenya kwa mujibu wa muumini Asya Salim, kadhi mkuu Shariff Ahmed Muhhar alitangaza kwenye vyombo vya habari mwezi umeonekana katika kaunti ya Wajir na hivyo ni ishara kwamba sikukuu ya Eid al Fitr ni Jumatano.

Wakati huo huo nchini Tanzania muumini Idrissa Omari alisema kwamba Mufti Sheikh Zuberi aliwatangazia waumini kupitia vyombo vya habari kwamba mwezi umeonekana jijini Dar es Salaam ikiwa pia ni ishara ya kukamilika kwa mfungo wa Ramadan.

XS
SM
MD
LG