Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 03, 2021 Local time: 16:48

Juhudi zaendelea kuiondoa Meli iliyokwama Mfereji wa Suez


Meli ya Ever Given iliyokwama katika Mfereji wa Suez

Meli kubwa ya mizigo bado imekwama katika mrefeji wa Suez kwa siku ya tano leo Jumamosi wakati mamlaka zinajiandaa kufanya  juhudi nyingine kuiondoa na kufungua tena njia hiyo ya mashariki na magharibi kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa duniani.

Meli ya Ever Given yenye bendera ya Panama ambayo imebeba mizigo kati ya Asia na Ulaya ilikwama Jumanne katika mfereji wa Suez unaopita kati ya Afrika na Peninsula ya Sinai.

Afisa mmoja wa usimamizi wa Suez ambaye hakutaka kutambulishwa amesema Jumamosi mamlaka zinatarajiwa kufanya majaribio mawili kuiondoa meli hiyo .

Hata hivyo mkuu wa mfereji wa Suez Luteni Jenerali Osama Rabei atafanya mkutano na waandishi wa Habari leo katika mji wa Suez kutoa maelezo zaidi ya operesheni hizo.

Taarifa zinasema Meli hiyo kubwa ya mizigo –inasababisha kukwama kwa biashara na bidhaa zenye thamani ya dola billioni 9.6 kwa siku, kulingana na takwimu za safari za meli.

Takwimu hizo zinaonyesha hasara ya dolla milioni 400 kwa saa moja katika biashara inayotokana na njia hiyo baina ya mashariki na magharibi.

Kampuni ya Lloyd’s inayofuatilia bidhaa zinazobebwa na meli inasema bidhaa inayopita katika mfereji wa Suez kuelekea nchi za magharibi ina thamani ya dolla bilioni 5.1 kwa siku wakati zile zinazo kwenda nchi za mashariki zina thamani ya dola billioni nne na nusu kwa siku.

Licha ya juhudi zinazoendelea kuikwamua meli hiyo, wataalam wanasema kazi hiyo inaweza kuchukua wiki kadha.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG