Katika taarifa, timu ya pamoja ya uchunguzi iliyojaribu kumkamata Yoon ilisema “ilikuwa haiwezekani kabisa” kuendelea na utekelezaji wa hati ya kumkamata iliyoidhinishwa na mahakama kwa kuzingatia upinzani na usalama wa wafanyakazi kwenye eneo la tukio.
Katika operesheni ya mapema asubuhi, timu ya wachunguzi na maafisa wa upelelezi, wakiungwa mkono na polisi wa kutuliza ghasia wapatao 3,000, walifika kwenye makazi ya Yoon katikati mwa Seoul, kama sehemu ya uchunguzi kuhusu uasi na matumizi mabaya ya madaraka.
Forum