Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 01, 2024 Local time: 23:48

Juhudi za kumaliza mzozo Ivory Coast zashindikana- Odinga


Mwakilishi wa umoja wa Afrika na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga.
Mwakilishi wa umoja wa Afrika na waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga.

Msuluhishi wa umoja wa afrika huko ivory Coast amesema juhudi zake za kumaliza mzozo wa kisiasa zimeshindikana na kuonya kwamba muda unakwisha kwa suala hilo kumalizika kwa amani.

Msuluhishi huyo waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga alifanya mikutano tofauti na marais wawili mahasimu wa Ivory Coast aliyeshikilia madaraka Laurent Bagbo na mpinzni wake Allasane Ouattara ambaye nchi nyingi zinamtambua kuwa ni mshindi wa uchaguzi wa rais wa Novemba.

Msuluhisihi huyo alionekana kumlaumu Bw. Bagbo akisema kwamba alivunja ahadi yake ya kuondoa vikosi vya usalama vinavyozingira hoteli ambayo, inatumika kama makao makuu ya muda ya Bw. Ouattara.

XS
SM
MD
LG