Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:24

Mwandishi wa habari auwawa Sudan Kusini


Wanafamilia na raia wakitazama mwili wa mwandishi Peter Moi, nje ya nyumba ya kuhifadhia maiti mjini Juba, Sudan Kusini, Agasti 20, 2015.
Wanafamilia na raia wakitazama mwili wa mwandishi Peter Moi, nje ya nyumba ya kuhifadhia maiti mjini Juba, Sudan Kusini, Agasti 20, 2015.

Mwandishi wa habari wa Sudan kusini amepigwa risasi na kupoteza maisha, siku tatu baada ya rais Salva Kiir kutishia kuuwa waandishi ambao kwa maneno yake “ wako kinyume na nchi”

Mtu mwenye silaha alimuuwa Peter Moi aliyekuwa mfanyakazi wa gazeti la The New Nation jumatano jioni karibu na ofisi hizo mjini Juba. Wafanyakazi wenzake wanasema inaonekana kuwa alilengwa kwa sababu mshambuliaji hakuchukua fedha za Moi wala simu yake ya mkononi.

Hakuna taarifa za awali kutoka jeshi la polisi au serikali. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry alizungumza na bwana Kiir kwa njia ya simu ili kuzungumzia tukio hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imeitaka Juba kufanya uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo. Moi ni mwandishi wa habari wa saba kuuwawa sudan Kusini mwaka huu. Jumapili rais Kiir aliwaambia waandishi wa habari mjini Juba kwamba, “ kama kuna mtu kati yao hafahamu kwamba nchi hiyo imeuwa watu , tutaonyesha siku moja, mara moja, na kwamba uhuru wa habari haumaanishi kufanya kazi kinyume cha nchi.

XS
SM
MD
LG