Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:21

Joto, moshi waongeza idadi ya vifo Moscow


Joto kali Russia pamoja na moshi wa moto wa porini wasababisha ongezeko la vifo katika mji wa Moscow.

Joto la majira ya kiangazi, ukame na moshi wenye sumu unaosababishwa na moto wa porini umesababisha ongezeko la vifo katika mji mkuu wa Russia - Moscow, mji wenye watu wengi kuliko yote barani Ulaya.

Vifo mjini Moscow vimeongezeka hadi wastani wa watu 700 kwa siku huku mji huo ukiwa unapambana na mchanganyiko wa viwango vya juu vya joto, na moshi wenye sumu kutoka misituni. Andre Seltsovky, mkuu wa afya Moscow amesema wiki kadhaa za joto kali na moshi unaosababisha hewa chafu ndio vimesababisha vifo hivyo.

Anasema wastani wa vifo mjini humo ulikuwa watu 360 hadi 380 kwa siku. Lakini Jumatatu wastani huo ulipanda hadi vifo 700.

XS
SM
MD
LG