Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 25, 2022 Local time: 20:46

Jordan yalipiza kisasi


Raia wa Jordan wakieleza ghadhabu yao juu ya kuuawa kwa rubani wao Muath al-Kaseasbeh. Feb.3, 2015

Video iliyowekwa kwenye mtandao ilimwonyesha rubani huyo Muath al-Kaseasbeh akiwa amefungiwa kwenye kizimba na kumwagiwa mafuta ya petroli na kisha kuchomwa moto akiwa hai.

Jordan imelipiza kisasi kwa kuwauwa wanamgambo wawili leo Jumatano, baada ya kundi la wanamgambo wa Islamic State kuuwa mmoja wa marubani wake.

Waliouawa ni pamoja na gaidi mwanamke Sajida al-Rishawi raia wa Iraq aliyehukumiwa kifo kwa kuhusika kwake katika shambulizi la bomu la mwaka 2005 mjini Amman.

Kundi la Islamic State lilikuwa linataka aachiwe huru. Nayo Jordan ikasema itamwachia pale tu rubani wake aliyetekwa nyara na na kundi hilo atakapoachiwa. Lakini iliibuka kuwa rubani huyo aliuawa kwa kuchomwa moto.

Jumanne, video iliyowekwa kwenye mtandao ilimwonyesha rubani huyo wa Jordan Muath al-Kaseasbeh akiwa amefungiwa kwenye kizimba na kumwagiwa mafuta ya petroli na kisha kuchomwa moto akiwa hai.

Aliuawa Januari 3 na alikuwa sehemu ya jeshi la muungano linaloongozwa na Marekani likifanya mashambulizi ya anga dhidi ya kundi hilo katili la Islamic State.

XS
SM
MD
LG