Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 25, 2024 Local time: 20:31

John Lewis akataa kuhudhuria ufunguzi wa Mississippi


John Lewis, kiongozi wa haki za kiraia na mbunge mkongwe Marekani.
John Lewis, kiongozi wa haki za kiraia na mbunge mkongwe Marekani.

Kiongozi wa haki za kiraia na mbunge wa siku nyingi nchini Marekani John Lewis hakuhudhuria ufunguzi wa nyumba ya makumbusho ya haki za binadamu siku ya Jumamosi katika jimbo la Mississippi kwa sababu Rais wa Marekani Donald Trump alikaribishwa.

Wakati huohuo katika Nyumba ya Makumbusho ya Waafrika wa Marekani ukumbi mwengine huko Jackson, Rais wa taasisi ya haki za kiraia Marekani, NAACP, Derrick Johnson alifanya mazungumzo na waandishi wa habari pembeni ambayo yalihudhuriwa na Mayor wa Jackson Chokwe Antar Lumumba.

John amesema kuwa kufanya shughuli hiyo pembeni ilikuwa na maana ya “ kutoa heshima kwa wale waliokuwa wamejitolea maisha yao kwa ajili ya haki za kiraia za watu wa Mississippi, ambapo Rais Donald Trump hakushirikishwa katika tafrija hiyo.

Nyumba ya makumbusho ya haki za kiraia katika mji wa Jackson huko Mississippi itakuwa na vielelezo vya harakati za umwagaji damu za waliopigiania haki za kiraia Marekani kutoka mwaka 1945 hadi mwaka 1976.

Nyumba hiyo ya makumbusho ya kale itajumuisha silaha za ugaidi na chuki wakati wa kundi la Ku Klux Klan na bunduki iliyotumika kumuuwa mwanaharakati Medgar Evers.

Rais Trump akitembelea nyumba mpya ya makumbusho huko Mississippi. Dec. 9, 2017.
Rais Trump akitembelea nyumba mpya ya makumbusho huko Mississippi. Dec. 9, 2017.

Miongo kadhaa baadae wakati Mississippi inaadhimisha miaka yake 200 jimbo hilo linatafakari historia yake iliyojaa mengi ya kutisha kupitia majumba mawili ya makumbusho yanayoonyesha pia minyororo ya utumwa, mavazi ya Ku Klux Klan na picha za michoro ya kunyon’gwa watu na ufyatuaji wa mabomu. Pia kuna makumbusho ya historia ya Mississippi ambayo yana vielelezo vya miaka 15,000 ya historia ya jimbo kutoka wakati wa zama za kale hadi hivi sasa.

Makumbusho hayo mawili ambayo yote yapo chini ya mwamvuli mmoja yamefunguliwa Jumamosi siku moja kabla ya maadhimisho ya miaka 200 ya Mississippi kuwa jimbo la 20 Marekani.

Lewis alisema katika taarifa yake kwamba “Kuhudhuria kwa Rais Trump na sera zake zenye maumivu ni dharau kwa picha za watu zilizowekwa katika makumbusho ya haki za kiraia”.

XS
SM
MD
LG