Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Juni 14, 2024 Local time: 18:02

Kerry ashutumu mashambulizi kwenye hospitali nchini Syria


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry aklizungumza kwenye kituo cha televisheni cha al_Hurra juu ya juhudi za waarabu katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry aklizungumza kwenye kituo cha televisheni cha al_Hurra juu ya juhudi za waarabu katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, John Kerry, ameelezea kughadhibishwa kwake juu ya mashambulizi ya anga kwenye hospitali moja ya watoto katika mji wa Aleppo nchini Syria. Akielekeza lawama kwa majeshi ya Rais Bashar al-Assad.

Shambulizi la anga la jana Alhamis liliharibu hospitali inayosimamiwa na kundi la madaktari wasio na mipaka, na kuuwa watoto wasiopungua 20 na madaktari katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi mjini Aleppo.

Shambulizi hilo la anga lilikuwa sehemu ya saa 24 za umwagaji damu mjini Aleppo ambapo zaidi ya watu 60 waliuwawa katika mapigano kati ya majeshi ya Syria na waasi. Kerry anatoa wito kwa Russia, mshirika mkuu wa Assad, kutumia ushawishi wake kumweleza asitishe mashambulizi.

XS
SM
MD
LG