Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 23:20

Joe Frazier, bingwa wa zamani wa ndondi afariki


Mhariri mkuu wa gazetti la The New York Daily News Kevin Convey (kulia) amkabidhi Joe Frazier (katikati) tunzo ya ukurasa wa kwanza wa gazeti la Daily News mwaka 2011.
Mhariri mkuu wa gazetti la The New York Daily News Kevin Convey (kulia) amkabidhi Joe Frazier (katikati) tunzo ya ukurasa wa kwanza wa gazeti la Daily News mwaka 2011.

Joe Frazier, bingwa wa zamani wa ndondi wizani ya juu anaekumbukwa kwa mapambano mapambano makali na ugomvi na Muhammas Ali, amefariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani ya ini.

Fraizer aliyekua pia akijulikana kwa jina la Smokin' Joe, aliyewaadhibu wapinzani wake kwa vikali akiwa katika ringi, alikuwa mwanabondia wa kwanza kumtandika na kumshinda bingwa mashuhuri wa wizani ya juu Muhammad Ali 1971.

Baadae alishindwa vibaya na Ali katika mapambano mawili na hakumpenda Ali kutokana na mdomo wake mkubwa akimuambia ni mtu mweusi anaeapigana kwa matumaini ya watu mweupe. Fraizer hakupenda hata kidogo makauli hayo na ugomvi wao umebaki kama tukio la kihistoria katika ubondia

Mapema mwezi Novemba mwakilishi wake wa biashara Leslie Wolff, aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba Fraizer yuko mahututi akiugua saratani ya ini.

Fraizer alishinda katika mapambano 32 akipata ushindi wa knockout mara 27 na kushindwa mara nne, mara mbli na Ali na mbili na George Foreman. Alikua bingwa wa kati ya 1968 hadi 1973.

XS
SM
MD
LG